Msanii Bright amefunguka kueleza sababu ya kuwashirikisha wasanii maarufu nchini katika nyimbo zake.
Bright ameiambia Metro FM ya Mwanza kuwa, “Ukiangalia kwenye wimbo wa ‘Nimemuona’ nimefanya na Belle 9 ili kutofautisha, watu wengi wanatufananisha mpaka muonekano wanasema sisi ndugu. Pia kwenye ‘Nitunzie’ nilikuwa nimerekodi kila kitu, nilipokuwa nasubiria mixing kwa Mr T, Barakah alipitapale akapendezwa na wimbo wangu akaomba namba kwa T, akanipigia simu akaniomba tufanye wote wimbo huo.”
“Amefanya kazi kubwa mashabiki wenyewe wameona ila haikuwa lengo mimi kufanya wimbo huo na Barakah. Ukizungumzia kwenye ‘Umebadilika’ sidhani kama ingeleta maana kama ningefanya mimi peke yangu kwa sasa hivi kwenye mazingira tunayoishi,” ameongeza.
Muimbaji huyo amesisitiza kuwa wimbo wake mpya ‘Umebadilika’ aliomshirikisha wote ameuandika yeye.

Tupia Comments: