Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wafanya kazi wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu wa fedha katika wizara zao.
Akijibu Swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Nnje kidogo ya mji wa Zanzibar Warizi wa Fedha na Mipango Dk.Khalid Salum amesema ni kweli kulitokea ubadhirifu wa Fedha katika wizara yake lakini tayari hatua za awali zishaanza kuchukuliwa.
Aidha amesema kwa wafanya kazi watakaobainika kushiriki katika ubadhirifu huo watachukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na makosa walioyafanya.
Udhadhirifu huo ulitokea katika Wizara ya Fedha umesababisha hasara ya Shillingi Billioni 1.1.
Tupia Comments: