Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu eneo la Manchester Arena nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo na ambalo liliua watu 22 na wengine 59 kujeruhiwa, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk Asha Roze Migiro amesema mpaka sasa hakuna mtanzania aliyeripotiwa kuathirika na shambulio hilo.
Balozi Dk Migiro alimweleza mwandishi wetu kwamba taarifa juu ya tukio hilo la kusikitisha bado zinaendelea kukusanywa na kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza anakutana asubuhi hii na Kamati ya Masuala ya Usalama na Maafa kupata tathmini ya tukio na hatimaye kulitolea taarifa rasmi.
Mpaka sasa haijafahamika nani wanahusika na utekelezaji wa tukio hilo lakini inasemekana limefanywa na mtu aliyejitolea mhanga na kwamba muhusika pia ni mmoja wa watu walikufa katika mlipuko huo.
Balozi Migiro imeleelezea masikitiko yake juu ya tukio hilo na kutoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zaidi kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi.
Tupia Comments: