Arusha. Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, ulipo mto Mlera.

Mkumbo ambaye yupo njiani akielekea wilayani Karatu amesema wanafunzi waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wa shule ya mchepuo wa Kiingereza, iitwayo LackVicent ya mjini Arusha.

Taarifa zaidi kuhusu tukuio hili zitaendelea kuwekwa hapa katika chumba cha habari cha kidijitali, MCL.

Tupia Comments: