Meli ya kivita ya Korea Kusini imetumwa katika pwani ya Somalia kushiriki katika mazoezi ya operesheni ya kijeshi ya kukabiliana na mabaharia ambao wameanza kuteka meli baada ya miaka kadha ya utulivu.
Meli hiyo kubwa yenye uzani wa tani 4,400 kwa jina Daejoyoung iliondoka katika bandari ya Busan nchini Korea Kusini jana kuelekea Somalia.
Meli hiyo ina mabaharia 300.
Mazoezi hayo ya Ijumaa yatashirikisha Daejoyoung, meli nyingine ya kibiashara ya uzani wa tani 17,000 pamoja na mabaharia 350, shirika la habari la Korea Kusini Yonhap limesema.
Taifa hilo limekuwa na wanajeshi katika Ghuba ya Aden tangu tangu 2009 ambapo wamekuwa wakishiriki kwenye juhudi za pamoja za jamii ya kimataifa za kukabiliana na maharamia katika pwani ya Somalia.
Uharamia kwenye maeneo ya maji pwani ya Somalia na Yemen, uliongezeka maradufu mwaka 2011, huku kukitokea zaidi ya mashambulio 200.
Lakini matendo hayo yalipungua pakubwa katika miaka ya hivi karibuni, baada ya kuongezeka kwa doria inayoongozwa na wanajeshi wa majini kutoka mataifa mbalimbali ya dunia, pamoja na uungwaji mkono wa wavuvi wa maeneo hayo wanaoendesha shughuli za uvuvi baharini.
Hata hivyo, sababu zilizowafanya wavuvi wengi wa Kisomali kutoroka kutoka maeneo ya pwani, na kuamua kuwa maharamia, yapata mwongo mmoja uliopita, bado zingalipo, anasema mwaandishi habari wa BBC wa maswala ya usalama Frank Gardner.
Kwa sasa Somalia inashuhudia hali mbaya ya ukame, umaskini umeongezeka mara dufu, huku vijana wengi wakiwa bila ajira.

Tupia Comments: