Jeshi la ivory cost
Mkuu wa jeshi nchini Ivory Coast amesema jeshi limeanzisha operesheni maalumu ya kurudisha hali ya utulivu katika mji wa pili kwa ukubwa wa Bouake ambao ulikuwa chini ya wanajeshi ambao wamekwenda kinyume na serikali kwa takriban siku ya tatu sasa.
Kumeibuka upinzani mkali dhidi ya wanajeshi hao wanaoonekana kwenda kinyume na maadili, hivyo kusababisha maandamano mapema hapo jana.
Watu sita wamejeruhiwa pindi wanajeshi waliporusha risasi kwa waandamanaji.
Kikosi hicho cha jeshi kimegoma kutokana na kutolipwa mafao yao hivyo kusababisha mji wa Bouake kutengwa huku maduka yakifungwa.
Wanajeshi hao wamesema hawataweka silaha chini.
Msafara wa magari ya jeshi unaelekea mjini humo.
Wanajeshi waasi wamezuia njia ya kuingia katika mji wa Bouake, ambao ndio kitovu cha uasi na pia eneo hilo ndilo lilikuwa makao makuu ya waasi pindi nchi hiyo ilipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wanajeshi walikuwa wakipiga risasi za tahadhari ili kufanya watu wabaki ndani pindi watu sita.
Haya yote yalianza siku ya Ijumaa asubuhi pindi wanajeshi waliokuwa katika kambi zao kuanza kupiga risasi hewani kupinga kusitishwa kwa makubaliano ya kuwalipa mafao kabla malipo hayajafanyika.
Rais Alassane Ouattara aliingia madarakani mwaka 2011
Hawa walikuwa waasi ambao walipigana kwa miaka kadhaa ili kumweka Rais Alassane Ouattara madarakani.
Wamesema hawatafanya mazungumzo yoyote na iwapo jeshi litaingilia basi watapigana.
Tupia Comments: