SOKO la Sabasaba Manispaa ya Dodoma linadaiwa kunufaisha wajanja wachache ambao wamekuwa wakijipatia mamilioni ya fedha kama kodi za pango huku manispaa ikiambulia ushuru wa Sh 200 kwa siku.

Hayo yalibainika wakati wa kikao cha baraza la madiwani katika manispaa ya Dodoma na kutaka suala la ukusanyaji mapato kufuatilia kwa makini. Soko hilo linadaiwa kuwa na vibanda 2,000 lakini vinavyotumika ni 1,200. Diwani wa kata ya Kikombo, Yona Kusaja, alisema halmashauri inapoteza fedha nyingi kwenye soko la Sabasaba huku wajanja wachache wakinufaika. Kusaja ambaye ameteuliwa kuwa mwenyekiti katika suala la kufuatilia soko hilo alisema soko hilo sehemu kubwa linamilikiwa na Manispaa na sehemu iliyobaki linamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Watu binafsi wanajipatia fedha nyingi kwa kukusanya kodi kubwa huku manispaa ikiambulia Sh 200 ya ushuru,” alisema Alisema soko hilo lilianza mwaka 1996 ambapo kulikuwa na majengo yanayotumika kama ofisi na sasa kuna ofisi ambazo zimepanga kwenye majengo yake. Alisema hapo awali majengo 23 yalikuwa yakitumika na Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Posta, Madini, Ujenzi, Afya Mkoa, Sido kanda, Umoja wa Wanawake (UWT) Bima, Shirika la Reli (TRC), Kampuni ya Bima (TBL) Ustawi wa Jamii Walemavu, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Kanisa la Wasabato (SDA).

“Kati ya vibanda 2000 vilivyopo kwenye soko hilo vinavyofanya kazi ni 1,200 ambapo vibanda na meza hutozwa Sh 200 kwa siku,” alisema. Alisema sehemu ya soko pia kuna maegesho ya mabasi na hiace za kwenda maeneo mbalimbali ya vijijini lakini hata ushuru unaokusanywa haijulikani unakwenda wapi.

“Hakuna rekodi zinazoonesha soko lina meza ngapi, mabasi, daladala ngapi vibanda vingapi pamoja na kiasi cha fedha kinachopatikana. Pia alisema soko hilo lina madalali na mafundi wa “Tunataka suala la ukusanyaji wa mapato liwe wazi ijulikane nani anapata nini na kwanini haiwezekani eneo lote lile manispaa ikose mapato” alisema Alisema kinachotakiwa kufanyika ni Manispaa kufuatilia majengo yote yanayoendeshwa chini ya usimamizi wa halmashauri na ifike wakati manispaa itoze kodi.

“Bora kuingiza kodi hiyo serikalini ili watu wasijinufaishe” alisema Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, alisema mapendekezo hayo ni mazuri. “Inapofika suala la kufuatilia mapato, wote tufunge mikanda kwenye utekelezaji huu, Diwani Kusaja ashirikishwe ili mwisho wa siku tuone halmashauri inapata mapato pale Sabasaba. Machi, mwaka huu Mwenyekiti wa soko hilo, Athumani Makole, alisema soko hilo siyo jipu wala mzigo na kuwaondoa hofu baadhi ya madiwani wa Halmashauri juu ya ukusanyaji wa mapato. Makole alisema soko hilo lipo kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wote na linakusanya mapato yake kwa lengo la kuinua uchumi manispaa, hivyo, hakubali sababu za madiwani kuliona kama ni jipu au mzigo katika halmashauri.

Tupia Comments: