Diego Costa ameacha mjadala mkubwa kwa mashabiki wake katika Twitter kutoka na ushangiliaji wake wa kupungia mkono alipofunga bao lake dhidi ya Middlesbrough ndiyo ishara ya kuaga Stamford Bridge.
Mshambuliaji huyo Mhispania anaonekana kama ataondoka Chelsea mwisho wa msimu huu inavyooneka atatimukia China.
Costa alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya Cesc Fabregas kabla ya kupitisha mpira katikati ya kipa Brad Guzan kufunga bao lake la 21 msimu huu.
Nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid alishangilia bao hilo kwa kupungia mkono wa kuaga wakati klabu yake ikiwa katika mazingira mazuri ya kutwaa taji la tano la Ligi Kuu England.
Marcos Alonso alifunga bao la pili akipokea pasi ya Cesar Azpilicueta na kupitisha mpira katikati ya miguu ya kipa Guzan kama alivyofanya Costa.
Nemanja Matic alifunga bao la tatu kwa Chelsea na kuielekeza Middlesbrough katika mlango wa kushuka daraja baada ya kipigo hicho cha mabao 3-0.
Tupia Comments: