Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein ametoa pole kwa wananchi wote Unguja na Pemba walio athirika na maafa ya Mafuriko yaliosababishwa na mvua za masika zinazoendelea nchini.
Akizungumza katika Ziara yake ya kukagua maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na mvua amesema Serikali yake imepokea kwa masikitiko taarifa za mvua ambazo zimewaathiri wananchi wengi hasa wanyonge ambapo amesema serikali haitokaa kimya juu ya maafa hayo.
Hata hivyo Amesema maandalizi yaliyokuwe hivi sasa kwa serikali ni kuyatengeneza na kukarabati maeneo yote unguja na pemba yalioathiriwa na mvua ili kuweza miundombinu kuwa bora na imara ili ili mvua zijazozisiweze kuharibu maeneo mengine.
Aidha Dr.Shein ametoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano wa kusaidia katika kipindi hichi cha mvua pamoja na kuwacha ukaidi walionao baadhi yao pale wanapoambiwa kuhama sehemu za mabondeni ili kunusuru maisha yao wananchi na mali zao.
Kwaupande wake mmoja ya wananchi walioathirika na mvua katika kijiji cha Bumbwi sudi kwagoa Issa Abdul-karibu amemuomba Rais Zanzibar wakati walipotembelewa katika kijiji chao kuwa kuharakishwe ukarabati wa mitaro iliyoziba kwani ndio chanzo cha mafuriko kutokea kwani mitaro hiyo haipitishi maji vizuri na imeziba kwa muda mrefu na kupelekea maji kuingia katika maazi ya wananchi ambapo kumesababisha wananchi kukosa makaazi ya kuishi
Ziara hiyo ya siku moja ya Dr. Sheini ilifanyika katika maeneo mbalimbali ambapo ni Mwanakwerekwe shimo la maji,Fuoni kibonde mzungu,Mwanakwerekwe nyumba mbili,Daraja bovu Karakana,Bumbwisudi kwa goa, Mwera Gudini na kesho ziara kama hiii itafanyika Kisiwani Pemba.
Tupia Comments: