Dar es Salaam.Wataalam wa afya katika masuala ya upasuaji wamekutana kujadili kuanzishwa kwa mpango kazi wa kitaifa utakaongalia kwa kina fani ya upasuaji.

Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha madaktari bingwa wa upasuaji, wataalam wa Wizara ya Afya na shirika la kimataifa la GE Foundation.

Rais wa Chama cha madaktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi Profesa Andrea Pembe alisema mpango kazi huo utaweza kuweka bayana ni wataalam wangapi wanahitajika kwenye upasuaji kuwatosha watanzania wote wenye uhitaji.

Amesema mpango huo pia utaangalia ni vifaa gani vya kisasa vinahitajika sambamba na dawa bora zitakazowezesha kuwatibu wagonjwa kulingana na mazingira yaliyopo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa GE Foundation Asha Varghest alisema lengo la kutengeneza mpango huo ni kuhakikisha mpango huo unazingatia mazingira halisi ya Tanzania na kuweka njia nzuri ya namna utakavyotekelezwa.

Tupia Comments: