Rais Magufuli leo wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amefunguka na kusema sasa anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya kufoji.
Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.
"Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda na kusema kwa kufanya hivyo itatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.
"Mtu amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani, akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa na saa zingine wakuu wa vyo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyo hivyo, sifahamu wanapangiwa kwa rushwa lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli
Tupia Comments: