Drogba anunua timu anayoichezea huko Marekani

New york, Marekani.DIDIER Drogba amekuwa mwanasoka wa kwanza anayecheza kumiliki timu baada ya kukubaliwa kuinunua klabu ya Phoenix Rising.

Straika huyo wa zamani wa Chelsea ameonyesha dhamira yake ya kuhamia Arizona, Marekani baada ya kushauriwa na bilionea mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.

Drogba, 39, alikataa ofa kibao za kuendelea kucheza kwenye Ligi Kuu England na alipewa pia nafasi na kocha Antonio Conte ili awemo kwenye benchi lake la ufundi. Lakini, ameamua kuwa mmoja kati ya watu kumi wanaoamua kuichukua Phoenix ili itambe kwenye Ligi Kuu Marekani.

Fowadi huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast, alisema suala hilo haliwezi kumlazimisha kocha, Frank Yallop, kwamba awe ana mpanga tu kwenye timu kwa sababu ni mmiliki.

Drogba alisema: “Majukumu ya kocha yataendelea kama yalivyo, nipo pale kama mchezaji. Hakuna namna yoyote nitakayoweza kumlazimisha kocha anipange. Siwezi kumwingilia uamuzi wake na wajibu wake.

“Kwa nafasi yangu ya kuwa pia mmiliki mwenzake, nitakachokuwa nazungumza ni suala la usajili mpya na nini klabu ifanye. Nitaendelea kucheza, lakini mipango yangu ni kuisaidia Phoenix kuwa timu kubwa kwenye MLS (Ligi Kuu Marekani).”

Kiwango cha Drogba enzi zake za uchezaji akiwa na Chelsea ndicho kitu kilichowavutia wachezaji kama Eden Hazard, Eric Bailly na Idrissa Gueye kuhamia kwenye soka la England.

Tupia Comments: