Diwani wa CHADEMA Kata ya Kitwiru katika Manispaa ya Iringa Ndugu. Baraka Kimata, alishikiliwa kwa muda na Jeshi la Polisi baada ya kutoa maneno yaliyotafsiriwa kwamba ni kashifa kwa mbio za Mwenge. Kimata ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Iringa Manispaa aliitwa Jukwaani kuongea kwa niaba ya chama chake baada ya Katibu wa CCM wilaya kuongea.
Kimata pamoja na mambo mengine aliyoongea, alimalizia hotuba yake kwa kusema kwamba kama CHADEMA ikipewa ridhaa ya kuongoza nchi basi wataupumzisha Mwenge wa Taifa. Baada ya hapo wasemaji wote waliofuatia akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Iringa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa walimshambulia Kimata na chama chake kwa msimamo huo wa kupinga Mbio za Mwenge.
Baadaye Kimata alikamatwa na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa na kuachiwa. Habari toka kwa watu walio karibu naye wanadai kwamba Kimata ametakiwa kuandika barua ya kuomba radhi kabla ya kesho saa kumi jioni.
Tupia Comments: