Mtangazaji wa kituo cha redio cha E-Fm na Mwanamitandao ya kijamii, Seth Katende maarufu kama “Bikira wa Kisukuma” amefariki dunia Jumapili hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akitibiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya EFM, Seth alifariki dunia baada ya kuugua ghafla kwa muda mrufi.
“Kwa masikitoko makubwa E FM inapenda kuwajulisha kuwa mwenzetu Seth Katende maarufu” Bikira wa kisukuma”amefariki dunia Leo mchana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili bmfupi. Seth atakumbukwa sana kwa ucheshi wake kupitia kipindi cha Ubaoni alichokua akiendesha sambamba na Imma Kapanga na Mpoki au “mwarabu wa Dubai”. Msiba upo nyumbani kwa baba yake mzazi Changanyikeni Dar es salaam.
Mmoja kati ya watangazaji wa EFM, Dina Marious ameeleza kusikitishwa na kifo hicho pamoja na neno la mwisho ambalo aliongea na marehemu kalba ya kifo chake.
“Tulikuwa wagonjwa wenza tumepishana wiki tu. Wewe umelazwa TMJ mimi nipo Sanitas kila siku lazima tuwasiliane tuchekiane vipi salama umeamkaje? kwemaa upande huo?Tupone bwana tukale firigisi,” aliandika Dina Instagram.
Aliongeza, “Simu yangu leo ilifichwa kwa muda nisielewe kinachoendelea wanaoniuguza wameuchuna mwisho ikabidi waseme tu.Kichwa kinaniuma sababu ya hali yangu lakini kimeongezeka maradufu kukulilia.Juzi unanipa moyo eti nitapona niende mtoto day Dah kumbe wewe hali imekuwa mbaya.#RIP SETH,”
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.

Tupia Comments: