Tayari klabu ya Everton  imethibitisha kumalizana na mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney kwa kumrejesha kwenye klabu hapo kwa mkataba wa miaka miwili.

Kupitia mtandao wa Klabu ya Everton taarifa zimesema wamefikia makubaliano hayo kwa mazungumzo ya muda mrefu na baada ya kutathmini uwezo wake na umri pamoja na uzalendo wake kwa klabu hiyo ambayo ndiyo imemkuza tangia akiwa na mika nane kabla ya kununuliwa na Man united mwaka 2004.

Dili la Manchester United kumchukua mshambuliaji wa Everton, Romelu  Lukaku limehusishwa pia na usajili wa nahodha huyo kipenzi cha mashabiki wa Man united, Wayne Rooney .

Tayari Rooney amekubali kujiunga na Everton kwa kupunguza mshahara wake wa wiki kutoka paundi 250,000 anazolipwa sasa na Manchester United mpaka 180,000 kiasi ambacho Everton wamekiri kukimudu.

Rooney kukubali kujiunga na Everton ni kujipatia tiketi ya kutembelea Tanzania kuja kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia alhamisi ya wiki lijalo (tarehe 13 julai).

Hii itakuwa fursa pekee kwa watanzania kumshuhudia nahodha huyo wa muda mrefu wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United kutua kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Mwishoni mwa mwezi juni afisa utawala na utekelezaji wa kampuni ya SportPesa nchini Abbasi Tarimba alisema kuwa  klabu ya  Everton imethibitisha kuleta timu yake ya kikosi cha kwanza nchini tanzania kitu ambacho kinatupa uhakika kuwa huenda hata Rooney akaja Tanzania wiki ijayo.

Tupia Comments: