Tanzania ilitoa wito Jumatano kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kusaidia kuwaokoa raia wake 21 waliotekwa nyara mwishoni mwa mwezi jana na waasi wa Mai Mai katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania, Mindi Kasiga, aliliambia shirika la habari la kitaifa kwamba raia hao 21 wa Tanzania, pamoja na Wakenya watatu, walikuwa wakiendesha malori yanayomilikiwa na kampuni zilizosajiliwa nchini Tanzania, walipotekwa nyara na Mai Mai, kundi la wanamgambo linalojumisha makabila mbali mbali, na ambalo limekuwa likipigana mara kwa mara na vikosi vya Kongo.
Hii si mara ya kwanza kwa madereva kutoka Tanzania kujipata mashakani nchini Kongo.
Mwezi Septemba mwaka jana, waasi wa Mai Mai walichoma malori manne na kuwateka madereva wanane wa Tanzania katika ejimbo la Kivu Kusini.

Tupia Comments: