Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo saa 2:30 usiku kutupa karata yake ya mwisho dhidi ya Lesotho kwa ajili ya kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano ya COSAFA mchezo utakaochezwa uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
Hatua hiyo ya Tanzania kukutana na Lesotho imekuja baada ya timu zote mbili kufungwa katika hatua ya nusu fainali ambapo Lesotho walichapwa 4-3 na Zimbabwe huku Taifa Stars kufungwa 4-2 dhidi ya Zambia.
Taifa Stars ilikutana na Lesotho Juni 10 katika mechi yao ya kirafiki iliyochezewa kwenye kwa wanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam na kutoka sare ya magoli 1-1.
Kwa upande mwingine, timu ya Zambia na Zimbabwe ndizo zitakazoweza kucheza fainali ya michuano hiyo Julai 9 mwaka huu.

Tupia Comments: