Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay saa moja iliyopita.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza majira ya saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.
Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.
Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.
“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.
Tupia Comments: