Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo Alhamis Julai 6,2017 saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu
Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.
Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi maiti yamemkuta.
Tupia Comments: