Polisi nchini Brazil wamamkamata mlanguzi wa madawa ya kulevya maarufu ambaye amefanyiwa upasuaji ili kukwepa kukamatwa kwa muda wa karibu miaka 30.
Luiz Carlos da Rocha ambaye pia anafahamika kama "White Head" anaamnika kuongoza genge kubwa la madawa ya kulevya barani America Kusini.
Polisi walisema kuwa hakuamu anayoweza kupewa Rocha inaweza kuwa ya karibu miaka 50 jela.
Rocha alikamatwa eno la Sorriso katika jimo la magharibu la Mato Grosson siku ya Jumamosi.
Amekuwa akiishi mjni humo akitumia jina Vitor Luiz de Moraes.
Polisi walilinganisha picha za zamani za Rocha na za mshukiwa ampya na kusema kuwa Luiz Carlos da Rocha na Vitor Luiz ni mtu mmoja.
Polisi wa Brazil wanasema kuwa genge lake lilitambuliwa kama lenye ghasia ambalo lilikuwa likitumia maghari yasiyopenya risasi na silaha nzito.
Genge hilo lilizalisha madawa ya Cocaine nchinin Bolivia, Peru na Colombia kabla ya kusafirisha madawa hayo hadi barani Ulaya na Marekani.
Tupia Comments: