Ndege ya kijeshi ya Urusi, Su-27 imefanikiwa kuitimua ndege ya jeshi la NATO, F16 ambayo ilikuwa ikiifukuzia ndege aliyokuwa amepanda waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu
Vyombo vya habari Urusi vimesema kuwa tukio hilo limetokea katika anga ya kimataifa eneo la Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda himaya ya Urusi ya Kaliningrad.
NATO baadaye ilisema ilifuatilia ndege hiyo kwa kuwa haikujitambulisha.
Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Urusi ndege ya F16 ilipita karibu na ndege ya Waziri wa Ulinzi, Shoigu, kisha ndege ya Urusi ya Su-27, ikaingilia kati na kutoa ishara kuonyesha kuwa ilikuwa imejihami, kisha ndege ya Nato ikaondoka.
Tupia Comments: