Serikali imetoa shilingi billion 4.7 kwa wakala wa majengo nchini tba ili kuanza rasmi ujenzi wa ikulu ndogo na ofisi za makao makuu ya mkoa wa songwe mradi unaoanza mara moja baada ya wananchi kujitolea eneo lenye ukubwa wa hekari 40 zilizopo katika mlima nselewa kata ya mlowo wilayani mbozi.
Mkoa wa songwe una zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kuanzishwa kwake lakini kwa kipindi chote hicho viongozi wa ngazi ya mkoa akiwemo mkuu wa mkoa wamekuwa wakifanya kazi kwa kujibana kutokana na kutokuwa na ofisi hali ambayo bi chiku galawa mkuu wa mkoa songwe amesema ilikuwa haitoi nafasi nzuri katika utendaji kazi ulio bora.
Aidha bi galawa amesema ujenzi huo utatosheleza kupatikana kwa ofisi za idara mbalimbali ngazi ya mkoa, nyumba ya mkuu wa mkoa na katibu tawala wake pamoja na ikulu ndogo na kwamba eneo hilo halina fidia kwa wananchi.
Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo tba elius mwakalinga amesema bajeti ya mradi ni sh. Billion 4.7, ambapo awamu ya kwanza itatumika billion 1.8 na kukamilisha boma ili ofisi zianze kufanya kazi, huku akitaja kuwa kupitia mradi huo miundombinu ya barabara, maji na umeme ambavyo havikwepo sasa vitapatikana.
Aidha kwa upande wao wananchi wa mkoa wa songwe ambao wamezungumza na ITV wamebariki makao makuu ya mkoa kujengwa karibu ndani kata ya Mlowo wakitaja kuwa hiyo ni fursa nzuri iliyorahisisha upatikanaji huduma za kimkoa ambazo awali baadhi yake zilifuatwa mkoani Mbeya.
Tupia Comments: