Huu ni wakati ambao Wakenya wanafuatilia kwa ukaribu kampeni za uchaguzi kupitia magazeti
Wafanyabiashara matajiri na mawakala wenye nguvu wa makampuni makubwa wameandaa mabilioni ya shilingi za Kenya kudhamini kampeni za kisiasa wakati mbio za kugombea urais zikitia kasi Jumamosi.
Wakati ushindani ukichukua sura mpya kuwapambanisha Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wa NASA, marafiki wa chama cha Taasisi ya Jubilee, inayompigania na kumuunga mkono Rais achaguliwe tena walifanya harambee ya chakula cha usiku kwa ajili ya kusaidia kampeni za chama hicho huko Safari Park Hotel. Usiku wa Ijumaa.
Jana, ilionekana kuwa NASA pia ilikuwa inamalizia matayarisho ya kufanya harambee ya kukusanya fedha katika chakula cha usiku huko Nairobi itayofanyika tarehe 19 June ambapo itafanyika sambamba na kuzinduliwa kwa ilani ya mseto wa NASA.
Kwa upande wa rais kuna mawakili, wamiliki wa mabenki, makampuni ya bima na mabilionea wafanyabiashara ambao wanajulikana katika duru za kisiasa na kibiashara nchini Kenya.
Kwa upande wa rais kuna mawakili, wamiliki wa mabenki, makampuni ya bima na mabilionea wafanyabiashara ambao wanajulikana katika duru za kisiasa na kibiashara nchini Kenya.
Katika kambi ya Raila kuna katibu uenezi bilionea Jimi Winjigi, ambaye amesifiwa kwa kuwaunganisha uongozi wa NASA kufikia mwafaka, Gavana wa Mombasa Hassan Joho—ambaye familia yake inamiliki wakala kubwa kuliko zote ya usimamizi wa mizigo bandarini, Gavana wa Nairobi Evans Kidero na aliyekuwa mkuu wa Bandari Kenya Brown Ondego.
NASA imesema kuwa harambee yake itaangaza kwa watu wa kawaida katika chama hicho. Musalia Mudavadi ambaye ni Mwenyekiti wa kampeni ya Urais ya NASA amesema mkakati wa NASA katika kuchangisha utahakikisha kuwa hauwekwi rehani na matajiri wakubwa endapo watashinda na kuchukua madaraka baada ya uchaguzi wa August 8.
Tupia Comments: