Vikosi maalum vya jeshi la Marekani vinasaidia vikosi vya ufilipino kupigana na makundi ya kigaidi ambayo yamezingira mji wa Marawi.
Makabailino hayo ya kuukomboa mji huo kutoka kwa wapiganaji wa Maute wanaohusishwa na kundi la Islamic state yameingia wiki ya tatu sasa.
Wanajeshi wa Marekani wanashiriki katika oparesheni hiyo miezi kadhaa baada ya kuwepo uhusiano mbaya kati ya rais Rodrego Durtete na Washington.
Mapigano ya hivi punde yamesababisha vifo vya wanajeshi 13 wa ufilipino.
Mamia ya wanamgabo wamekuwa wakipeperesha bendera ya kundi la Islamic State.
Mauaji hayo ya hivi punde ya wanajeshi wa ufilipino yamefakisha idadi yote wya wanajeshi wa Ufilipino waliouwa kwenye mapigano kuwa 58.
Takriban wanamgambo 138 na raia 20 pia wameuwa, kwa mujibu wa serikali.
Mji wa Marawi uko katika kisiwa cha kusini cha Mindanao ambao una waislamu wengi katika nchi hiyo yenye wakatoliki wengi.

Tupia Comments: