Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa ameunda tume huru ya kuchunguza suala la mama ambaye amedai kuibiwa mtoto wake katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.
Mwanamke huyo aitwae Asma Juma Elius mkazi wa Dar es salaam kudai kuibiwa mtoto ambaye inadaiwa wakati akifanyiwa Ultra sound alikua na ujauzito wa Watoto mapacha lakini baada ya kujifungua aliambiwa amejifungua mtoto mmoja.
Kufuatia sakata hilo Waziri Ummy ameamua kuingilia kati kwa kuunda Tume ya Wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuchunguza na kubaini ukweli.
“ Nikiwa kama Waziri mwenye dhamana, na wajibu wa kutenda haki nimeamua kuunda timu huru ya kuchunguza suala hili ambayo itaongozwa na Prof. Charles Majinge – daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti.”
Tupia Comments: