Wagonjwa wakisumbiri hospitalini Indonesia baada ya mfumo wa hospitali kuathiriwa na udukuzi.
Wataalamu wa usalama wa mitandao wanakubali ushahidi wa kifundi unaofungamana na Korea Kaskazini na shambulizi la uhalifu wa mitandao wa kimataifa unaojulikana kama WannaCry “ransomware”.
Hata hivyo mpaka Jumanne kwa namna fulani ushahidi uliopo ni dhaifu, lakini Pyongyang bado inauwezo wa juu katika masuala ya kimitandao na pia kila sababu ya kutafuta fidia kwa kupoteza kipato chake kutoka na vikwazo vya kiuchumi, na hivyo kuwa mshukiwa mkuu.
Tangia Ijumaa, kirusi cha WannaCry kimeathiri zaidi ya kompyuta 300,000 katika nchi 150, kikisababisha kusimama mifumo ya viwanda, mabenki, idara za serikali, mahospitali na usafiri dunia nzima.
Jumatatu wachambuzi wanaohusika na makampuni ya usalama wa mitandao, maabara ya Symantec na Kaspersky wamesema kuwa baadhi ya programu iliyotumika katika kirusi cha awali cha WannaCry kimeonekana katika programu inayotumiwa na Kikundi cha Lazarus Group, ambacho kimetambuliwa na baadhi ya wataalamu wa viwanda kama ni operesheni ya udukuzi ya Korea Kaskazini.
“Hivi sasa tumegundua baadhi ya kile tunachoweza kukiita ni viashiria dhaifu au viunganishi dhaifu kati ya WannaCry na kikundi hiki ambacho siku za nyuma kilikuwa kinajulikana kama Lazarus. Lazarus ilikuwa, kwa mfano tu, nyuma ya shambulizi la Sony na mabenki ya Bangladesh.
Lakini dalili hizi hazitoshelezi kwa kukuhitimisha moja kwa moja kwamba ni Lazarus ndio wahusika pekee,” mtafiti wa Symantec Eric Chien amesema.
Hata hivyo Symantec amelihusisha kundi la Lazarus kwa mashambulizi kadhaa ya mitandaoni katika mabenki ya bara la Asia ikiendea hadi miaka ya nyuma kabisa, likiwemo shambulizi lililo husisha wizi wa kidigitali wa Dola za Marekani milioni 81 kutoka benki kuu ya Bangladesh mwaka jana.
Serikali ya Marekani imeilaumu Korea Kaskazini kwa udukuzi wa picha za kampuni ya Sony ambazo zilivujishwa na kuathiri taarifa binafsi baada ya Pyongyang kutishia kuchukua “hatua za kulipiza” iwapo studio hizo zitatoa filamu za vichekesho (Zilizokuwa na kiza) zinayoonyesha kuuawa kwa Kim Jong Un.
Pia Korea Kusini iliituhumu Korea Kaskazini kwa kujaribu kuharibu usalama wa mitandao wa mabenki yake, vituo vya matangazo na vituo vya kuzalisha umeme katika vipindi tofauti.
Pyongyang inasadikiwa kuwa ina maelfu ya wataalamu wa juu wa kompyuta ambao wanafanya kazi katika kitengo cha vita vya mitandao kinajulikana kama Bureau 121, ambayo ni sehemu ya kitengo cha uchunguzi, kinachohusika na shughuli za ujasusi kinachoendeshwa na jeshi lake.
Tupia Comments: