Wasichana 82 wa shule ya Chibok ambao waliachiwa huru na wapiganaji wa Boko Haram majuma mawili yaliyopita, wamepatanishwa rasmi na wazazi wao, katika hafla iliyojaa majonzi, vilio na furaha
Hii ni mara ya kwanza kwa wasichana hao kukutana na jamaa zao, tangu walipotekwa nyara na wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Waliimba na kucheza, wakati wazazi wao walipokuwa wakishuka kutoka ndani ya mabasi ambayo yaliwasafirisha usiku kucha kutoka Chibok, kaskazini mashariki mwa mji mkuu Abuja.
Wazazi wao waliwabusu, huku machozi yakitiririka kwenmye nyuso zao, ilihali baadhi yao walilia kwa sauti, na kumshukuru maulana.
  • Msichana wa Chibok akataa kurudi nyumbani
  • Buhari na Wasichana wa Chibok
  • Video 'yaonyesha wasichana wa Chibok waliotoweka
Wasichana hao wangali wakitibiwa na kupewa mafunzo nasaha na ushauri wa kisaokolojia, kabla ya kukubaliwa kwenda nyumbani na kurejeshwa shuleni.
Serikali ya Nigeria inaendelea kujadiliana na kundi la Boko Haram ili liwaachie huru zaidi ya wasichana 100 wa Chibok ambao wangali wakizuiliwa.

Tupia Comments: