Rappa Stamina anaye-hit kwa sasa na ngoma ya 'Love Me' amefunguka na kudai ameamua kuimba wimbo wa mapenzi, siyo kwa sababu nyimbo zake ngumu zimebuma bali amebadilika kidogo ili kuimba vitu vilivyopo kwenye jamii kwa kuwa yeye ni msanii.
Stamina amefunguka hayo mbele ya kamera za eNewz na kudai kwamba ujio wake mpya ameamua kuimba maisha yaliyopo kwenye jamii inayomzunguka na kuongeza kuwa hajatoa kwa sababu ameumizwa kimapenzi bali yeye kama msanii ni wajibu wake kwa kuwa mapenzi ni maisha yaliyopo kwenye sehemu jamii.
Akizungumza kuhusu kuimba mapenzi kitu ambacho siyo kawaida yake, Stamina amesema "Hakuna kitu kigumu mbele ya mapenzi kwani hata wana hip hop tuna hisia kama watu wengine. Sijatoa 'Love me' kwa sababu nimetendwa ila nimeimba kuwasilisha kazi ya sanaa kwa sababu mimi ni msanii. Mwana hip hop akitoa nyimbo ya mapenzi watu wanamshangaa kwani sisi ndio hatuna wapenzi? mapenzi ni sehemu ya maisha" Stamina alifunguka.
Kwa upande mwingine rappa huyo ambaye amemshirikisha Maua Sama katika wimbo wake mpya amefunguka na kusema kwamba hakuna wimbo wowote duniani unaobuma kwenye game bali mapokezi ndiyo husababisha kazi kuwa hit au kuonekana kawaida.
"Hakunaga ngoma inayobuma duniani, kwa sababu ngoma wewe unayohisi imebuma kwako kwa mtu mwingine ni kali sana na kwenye simu yake utakuta ndiyo anaisikiliza sana. Ila kinachotokea ni ngoma kushindwa kufika mahali palipotarajiwa na wakati mwingine siyo lazima zote zifike. Kitu kama hit inatokeaga tu kutokana na mapokezi ya watu' Stamina aliongeza.
Tupia Comments: