Mfalme wa Saudi Arabia Salman Bin Abdulaziz amemtunukia Rais wa Marekani Donald Trump nishani ya kiraia ya juu kabisa ya ufalme huo.
Nishani hiyo imetolewa Jumamosi wakati walipokutana kwenye Kasri ya Mfalme katika mji mkuu wa Saudi, Riyadh.
Baada ya Trump and wengine kuingia katika ukumbi huo huku muziki wa bagpipes ukipigwa, King Salman alimvisha rais medali ya dhahabu ya King Abdulaziz al-Saud.
Trump aliwasili Riyadh Jumamosi kuanza ziara yake ya kigeni katika wadhifa wake wa urais.
Rais na mkewe Melania walilakiwa uwanja wa ndege na Mfalme Salman. Mfalme na Trump na mkewe walitembea katika zulia jekudu kuingia katika Ukumbi wa Kifalme, ambayo ni sehemu ya jengo la uwanja wa ndege ambapo walifanya mazungumzo mafupi.
Dakika chache baadaye, Trump pamoja na Mfalme wa Saudi waliondoka uwanja wa ndege katika magari maalum, wakielekea jijini kupitia njia ambazo zilizokuwa hazina msongamano wa magari.
Kulikuwako na ulinzi mkali katika maeneo ya uwanja wa ndege ambapo magari ya kijeshi yaliosheheni silaha yalikuwa yakifanya ulinzi.
Saudi Arabia sio nchi ambayo rais wa Marekani aghlabu anaikusudia katika ziara yake ya nje ya kwanza. Lakini Trump amefanya ni kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya kwanza ya kirais nchi za nje.
Hili limewashangaza zaidi wengi katika kile ambacho amekuwa akikipigia debe “Marekani Kwanza” kisiasa na katika matamko yake ya kampeni akitaka katazo la waislamu lililofuatiwa na amri za kiutendaji ambazo zilikuwa zinapiga marufuku nchi sita zenye Waislamu wengi kuingia Marekani
Saudi Arabia, ambayo inaushirikiano na mafungamano makubwa ya siku nyingi na Marekani katika nishati na ulinzi ilikuwa haijatajwa katika katazo la kusafiri la Trump.
Tupia Comments: