Siku 9 zimepita tangu itokee ajali iliyoleta simanzi kwa Taifa zima la Tanzania na Dunia kwa Ujumla, ajali hiyo ilihusisha basi dogo la Wanafunzi na kukatisha uhai wa wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1, huku ikiacha majeruhi 3 ambao wanatibiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha, Mount Meru.
Kwa kushirikiana na Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kumewezesha kupatikana msaada wa kuwapeleka majeruhi wa ajali hiyo nchini Marekani kutibiwa bure na tayari ndege maalum yenye uwezo wa kufanya kazi kama Ambulance imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuwachukua majeruhi hao.
Ndege hiyo ijulikanayo kama Samaritan Purse DC 8 N782SP imewasili jana May 13 ikiwa na Marubani wanne na Wahudumu wake 7 tayari kuwabeba Majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwenye matibabu.
Rubani wa Ndege hiyo amewaambia Waandishi kwenye uwanja wa ndege Kilimanjaro (KIA) kwamba wataondoka leo May 14 na watasimama Cape Verde kuweka mafuta na kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia jumatatu usiku.
Tupia Comments: