MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambazo kitaifa zinafanyika leo mjini Moshi
Samia aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana jioni, wakati Rais Magufuli na Waziri Mkuu waliwasili tangu juzi wakitokea mkoani Dodoma.
Rais Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zinazofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani hapa iliyoanza juzi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, Rais Magufuli atazungumza na wafanyakazi wote nchini kupitia sherehe hizo kwenye uwanja huo.
Aidha, inatarajiwa kuwa pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli atatoa maelekezo kuhusu kilio cha vyama vya wafanyakazi ambacho ni pamoja na kukosekana kwa mikataba ya hali bora kazini.
"Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika kilele cha sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo kwa mwaka huu zinafanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Pia nashauri wafanyabiashara watumie fursa hii kufanya biashara zako kwa ukarimu na uaminifu mkubwa ili kuwavutia wageni wanaoingia Moshi na watakaoendelea kuja," alisema Sadiki
Tupia Comments: