Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema serikali inatarajia kupokea magari zaidi ya 200 nchini ambayo yatagawiwa katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji mkubwa wa katika shughuli za doria na kuimalisha ulinzi na usalama
Mwigulu amebainisha hayo wakati akijibu Bungeni Mjini Dodoma kuhusu mpango wa serikali wa kutatua changamoto wanazopata askari wa jeshi la polisi kuhusiana na uhaba wa mafuta na magari hasa katika kipindi hiki kigumu cha askari kupambana na uhalifu.
"Bajeti hii tuliyopitisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya mafuta, doria pamoja na shughuli zingine imeongezeka tofauti ilivyokuwa inatoka awamu ya kwanza mwaka wa fedha uliopita, kwa maana hiyo tutakuwa tumepunguza changamoto kubwa ya ukosefu wa mafuta katika shughuli zetu za doria". Alisema Mwigulu
Vile vile, Waziri aliendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema "Mwaka jana tulipokea magari 77 kwa ajili ya askari wetu na kati ya mwezi huu (Mei) mpaka wa saba (Julai) tunategemea kupokea magari mengine zaidi ya 200 na tutayagawa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa kwa ajili ya shughuli za doria ikiwemo mikoa ya Kagera, Kigoma, Katavi pamoja na maeneo mengine ambayo wanahitaji magari hayo kwa ajili ya doria katika sehemu zao".
Tupia Comments: