Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora ikiwa ni siku chache tu, tangu Rais wa Korea Kusini kusema yupo tayari kwa mazungumzo.

Kumekuwa na shutma kubwa kote duniani dhidi ya hatua ya hiyo ya Korea Kaskazini, kufanyia majaribio yake zana za nuklia

Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe taifa hilo huku Ikulu ya White House ikisema kuwa, Pyongyang imeachwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu.

Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini, cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama kitendo cha uchochezi.

Jeshi la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya Japan.

Moon ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri wake wa kiusalama.

Jaribio lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba wiki mbili zilizopita.

Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na vikwazo na kufanya majaribio matano ya zana zake za masafa marefu za nuklia.

Chanzo: BBC

Tupia Comments: