Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliao mh Edwin ngonyani amezinduwa usafiri wa ndege mpya aina ya bombandier mkoani tabora yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 76 kupitia shilika la usafiri wa anga la (AIR TANZANIA COMPANY LIMITED) Kupitia uziduzi huo Naibu waziri amesema kuwa hiyo ni mojawapo ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa jamhuli ya muungano wa tanzania Mh John pombe magufuli wa kuboresha usafiri wa anga na wa garama nafuu na ndege hiyo itafanya usafiri kutoka Tabora kwenda Dodoma, Tabora kwenda dar es salaam kwa haraka zaidi na kusema kuwa ndege hiyo imenunuliwa kwa jasho la wananchi hivyo basi ndege hiyo ni mali ya wananchi wa tanzania hiyo nawaomba wananchi muweze kutumia ndege hii,
Mkuu wa mkoa wa Tabora mh Mh. Aggerey Mwanri amesema kuwa hiyo ni neema kwa wananchi wa mkoani hapo hivyo anatowa shukulani kwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh magufuri kwa kuitekeleza ahadi yake mungu amubaliki saana na kuwahimiza wananchi kuiona hiyo fursa na kuitumia ipaswavyo

Tupia Comments: