MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezman amedokezea uelekeo wake Manchester United akisema zimebaki hatua nne za kukaribia Old Trafford kati ya 10.
Griezmann anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa Ligi Kuu England, kiasi cha Pauni 295,000 kwa wiki na uhamisho wake unaweza kugharimu Pauni Milioni 80 kutoka klabu hiyo ya Hispania. Griezmann, mwenye umri wa miaka 26, amesema; "Nafikiri mustakabali wangu utaamuliwa wiki mbili zijazo,".
Alipoulizwa kama United ndiyo kitakuwa kituo chake kifuatacho, akasema; "Inawezekana. Naweza kukupa uhakika wa sita kati ya 10,".
Na kuhusu kubaki Atletico Madrid, Griezmann akasema: "Kuna saba kati ya 10 ya nafasi ya kubaki,".
Inafahamika ushindi kwa United dhidi ya Ajax katika fainali ya Europa League utawahakikishia nafasi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao, hivyo watajiongezea nafasi za kumpata mchezaji huyo.
Griezmann, anayevaa jezi namba 7 Atletico na timu ya taifa ya Ufaransa, pia alizungumzia namna anavyovutiwa na gwiji wa zamani wa Manchester United na England, mvaa namba 7 maarufu enzi zake, David Beckham
Tupia Comments: