Zaidi ya watu 90 wahofiwa kuzama baharini Libya
Mashua moja iliyokuwa na karibu wahamiaji 120 imezama nje ya pwani ya Libya kwa mujibu wa mkuu wa ulinzi pwani eneo hilo.
Zaidi ya watu 90 wanahofiwa kuaga dunia lakini shughuli ya kutafuta na kuokoa bado inaendelea.
Njia za baharini kuingia kusini mwa Ulaya zimekuwa maarufu zikutumiwa na wahamiaji, wakimbizi na watafuta hifadhi.
Msemaji wa kikosi cha ulinzi pwani mwa mji wa Tripoli Ayoub Kassem, anasema anaamini kuwa kila mtu ambaye alikuwa katika mashua hiyo alitoka nchi za kusini mwa jangwa la sahara.
- Wahamiaji 200 wafa maji baada ya boti kuzama
- Wahamiaji waokolewa pwani ya Libya
- Wahamiaji wasio na vibali wakamatwa Marekani
Ni watu 23 katika ya takriban watu 120 waliokolewa baharini mapema leo.
Manusura wamepelekwa katika kituo cha kuwazuia kilicho uwanja wa ndege wa Maitiga.
Manusura hao pia wanasema kuwa wale wanaoaminiwa kuzama ni pamoja na wanawake na watoto.
Tupia Comments: