Doha,Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis amekutana na Kadhi mkuu wa Qatar leo Jumamosi wakati wa ziara yake katika taifa hilo tajiri kwa mafuta la Ghuba na ambako kuna kambi kubwa ya vikosi vya anga vya Marekani Mashariki ya kati. Ziara ya Mattis nchini Qatar ni sehemu ya ziara yake katika ukanda huo ambapo pia amezitembelea Saudi Arabia, Misri na Israel kabla ya kuitembelea Djibouti hapo kesho Jumapili. Mkutano wa mkuu huyo wa wizara ya ulinzi na Kadhi Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani, unanuia kuimarisha mahusiano baina ya mataifa hayo mawili. Mazungumzo yao yalitarajiwa kulenga mapambano dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu IS, mzozo wa Syria na wajibu wa kikanda wa Iran, ambao Mattis ameuelezea kuwa umekosa uthabiti. Mahusiano ya serikali ya Marekani na taifa hilo yalitetereka wakati wa utawala wa Rais Barack Obama ambapo viongozi wake walisita kuingilia kati vita ya Syria.

Tupia Comments: