MOSCOW, Vikosi vya usalama nchini Urusi vimewaua wanamgambo wawili waliokuwa na silaha na kupatiwa mafunzo na kundi la Dola la Kiislamu IS na walikuwa wakijipanga kufanya mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi. Kamati ya kitaifa ya kupambana na ugaidi imesema wanaume hao wawili wameuawa katika mkoa wa kusini mwa Urusi baada ya kufyetuliana risasi na vikosi vya usalama ambavyo vilijaribu kusimamisha gari lao.
Taarifa zaidi zinasema mmoja wa wanamgambo hao ni kiongozi wa kundi la kigaidi aliyepatiwa mafunzo katika makambi ya IS na baadae kurejea Urusi ili kufanya vitendo vya ugaidi, shirika la habari la Interfax limenukuu taarifa ya kamati hiyo. Urusi imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujiripua na kuwaua watu 16 katika kituo kikubwa cha treni za chini ya ardhi cha St. Petersburg hivi karibuni.
Tupia Comments: