Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Joyce Mukya, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu, Mhe. Antony Mavunde amesema serikali itawachukulia hatua waajiri wote wanaofanya udhalilishaji wa namna hiyo.

Huku akieleza kuwa serikali imekwisha toa maagizo ya namna ya kufanya ukaguzi bila ya kudhalilisha utu wa mtu.

Mbunge wa viti maalum Joyce Mukya aliilalamikia kampuni ya madini ya Tanzanite One kwa kuwa na tabia ya kuwakagua kinyume na maumbile wafanyakazi wa migodini, jambo ambalo serikali imeahidi kuchukua hatua.

Tupia Comments: