Taarifa kutoka Somalia zinaeleza kuwa mizinga kadha imerushwa dhidi ya uwanja wa ndege katika mji mkuu, Mogadishu.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema askari wa usalama wa Somalia, walipambana kwa risasi, na washambuliaji.
Inafikiriwa msha-mbu-liaji mmoja aliuwawa. Haijulikani nani alihusika na shambulio hilo.
- Shambulizi la bomu laua watu 10 Mogadishu
- Amri ya kutotembea yatangazwa Mogadishu
- Watu 30 wauawa kwenye shambulio Mogadishu
Wakati huohuo, Shirika la Chakula Duniani, WFP, linasema kumetokea mlipuko mita mia moja kutoka msafara wake mjini Mogadishu.
WFP inachunguza kama mlipuko huo ulilengwa dhidi ya msafara wake.
Tupia Comments: