Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limeungana na mashirika mengine yanayotaka shitaka la uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Zambia na wenzake watano kufutiliwa mbali mara moja na kusema, ni kampeni ya mateso .Hakainde Hichilema alikamatwa baada ya kukataa kuupisha njia msafara wa rais Edgar Lungu,Kitendo kinachoonekana kama utovu wa adabu kwa rais.
Hakainde pamoja na wenzie watano ambao ni wajumbe wa chama cha United Party for National Development wamekuwa wakishikiliwa kwa zaidi wiki mbili kwa kile Amnesty ilichosema ni kosa la usalama wa barabarani na sio uhaini.
Pia Amnesty imetaka kuchunguzwa kwa tuhuma za kuteswa kwa kiongozi huyo na watu waliokuwa wamejifunika nyuso.Mashtaka ya uhaini yanaonekana kama njia moja wapo wa rais ya kunyamazisha upinzani, baada ya uchaguzi uliopingwa ambao uliambatana na vurugu.
Kwa upande wake, kiongozi huyo wa upinzani amekuwa akijitetea kwamba waliruhusiwa kuupita msafara wa rais na mamlaka kwa sababu walikuwa wakienda kwenye shughuli ya kidini.

Tupia Comments: