Dar es Salaam.Waziri wa  Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto,Ummy Mwalimu amesema Serikali  imedhamiria kushirikiana na wadau wa Himophilia katika kufikisha elimu ya uenezi kwa jamii nzima  ili kuwajengea uelewa juu ya ugonjwa huo.

Himophilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda.Ugonjwa huu pia hurithiwa na huwakumba wanaume na wanawakae na una changamoto nyingi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo  (Jumanne)katika hotuba yake iliyosomwa na Mtaalamu wa Afya na Magonjwa yasiyoambukizwa wa wizara hiyo, Profesa Ayub Magimba wakati akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya ugonjwa wa Himophilia.

Amesema mbali na wadau hao pia wizara yake itashirikiana na asaso nyingine  na masharika yasiyo ya kiserikali  katika kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo,sanjari kuhakikisha  huduma za matibabu yake zinaimarika.

Tupia Comments: