Mauji ya "halaiki" yameanza tena Sudan Kusini
Upo wasiwasi mkubwa kuwa mapigano yanayoendelea kwa sasa nchini Sudan Kusini ni mauji ya Kimbari ambayo yanafanywa kwa misingi ya kikabila amesema waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Priti Patel.
Upo wasiwasi mkubwa kuwa mapigano yanayoendelea kwa sasa nchini Sudan Kusini ni mauji ya Kimbari ambayo yanafanywa kwa misingi ya kikabila amesema waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Priti Patel.
Waziri Patel amewataka viongozi kutoka mataifa ya kigeni kufanya juhudi zaidi kuishinikiza serikali ya Sudan Kusini kuumaliza mgogoro ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu. Akizungumza na waandishi wa habari punde baada ya kukamilisha ziara yake katika taifa hilo changa zaidi duniani, waziri huyo wa Uingereza alisema alichokiona ni cha kusikitisha, kuanzia msako wa nyumba hadi nyumba kuwatafuta na kisha kuwaua wapinzani wa serikali hadi kuteketezwa vijiji wanamoishi. Akinamama katika vijiji hivyo pia wamebakwa huku serikali ya rais Salva Kiir ikitumia chakula kama silaha ya vita, kwa kuzuia chakula cha msaada kufika maeneo ya upinzani. Waziri huyo pia alitembelea kambi kadhaa nchini Uganda zilizowapa hifadhi zaidi ya wakimbizi lakini nane wa Sudan Kusini. Maelfu ya wakimbizi wanaendelea kuvuka mpaka kufuatia ripoti za mauji ya kikabila.
Wasudan Kusini wanaotoroka vita
Wakimbizi hao wanasema mashambulizi ya sasa yanafanywa na vikosi vya serikali kutoka kabila la rais Salva Kiir la Dinka na yawalenga watu wa kabila la aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar la Nuer. Watu kutoka makabila mengine madogo wanaoshukukiwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali, pia wamekuwa wakilengwa katika mashambulizi hayo. Password Okot ni mmoja wa wakimbizi hao,“Nilikuwa na ndugu wawili; mmoja wao alikamatwa na askari na kuchinjwa bila sababu. na mwingine alikuwa akijaribu kutoroka lakini akapigwa risasi. Mimi sijui nifanye nini na wake zao na watoto.Bado niko katika hali ya mshtuko na huzuni nyingi hivi sasa.Nimefikiria hata kurejea tena katika kijiji changu ili mimi pia niuliwe .Ni uchungu usioweza kustahimilika.”
Viongozi wa Afrika wasalia kimya
Wakati wa ziara yake nchini Sudan Kusini waziri wa Uingereza pia alikutana na rais Salva Kiir. Patel amewakosoa viongozi wa Afrika kwa kutoishinikiza serikali ya Sudan Kusini kusitisha mauji na machaufuko, badala ya kusubiri ufumbuzi kutoka mataifa ya bara jingine.
Waziri wa maswala ya kigeni Ujerumani Sigmar Gabriel
Ujerumani ni miongoni mwa mataifa yaliyotoa usaidizi wake Sudan Kusini hasa kwa wanaokabiliwa na njaa kama asemavyo waziri wa maswala ya kigeni Ujerumani Sigmar Gabriel.“Sisi tunafanya hivi kutokana na mahitaji ya msaada wa kiutu,na pia kwasababu tunaamini ni swala la heshima kuwa bara ulaya, kuwa mjerumani na pia jukumu letu la kuwajibika katika jamii ya kimataifa kwa kutoa usaidizi ili kuhakikisha angalau watu wanasalimika.”Shirika la Umoja wa mataifa linakadiria watu wapatao millioni tatu wametoroka makwao kutokana na vita hivyo huku wengi wao wakipata hifadhi katika taifa jirani la Uganda.
Tupia Comments: