Jana Bungeni Dodoma, Joshua Nasari(Mb) Arumeru Mashariki amekamatwa na Watu wa Usalama akiwa amelewa huku akiwa na chupa akitaka kuingia nayo Bungeni.
Mb Joshua alipoanza kuchangia alisema kuwa kamati iliyoundwa na Bunge wakati ule wa Rais Kikwete, kumchunguza Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa juu ya tuhuma za Richmond haikutenda haki kabisa.
Akijibu tuhuma hizo kwa kujiamini kabisa, Mh. Harrison Mwakyembe alisema yafuatayo:
"Kwanza niwashukuru vijana wa Usalama kwa kutekeleza majukumu yao hasa ya kumshika Mh. Nasari na chupa hiyo ya kilevi, maana angeweza kutapikia bendera ya Taifa hivyo kulidhalilisha Bunge lote kwa ujumla...
Kuhusu Edward Lowassa na tuhuma hiyo ya Richmond hawezi kusafishika kamwe kwa hali yoyote ile...Tumeshawachoka sana na hatuwezi kuwavumilia tena....
Kamati yangu iliwahoji zaidi ya mashahidi 75,huku kabla ya kuhojiwa kwake na kamati hiyo Edward Lowassa alikimbilia kujiuzuru ghafla...Sasa bhasi kama kuna mtu yeyote hapa Bungeni anayejiamini alete hoja ya kurudisha tuhuma hizo za Richmond kuhusu Edward Lowassa tuanze kuijadili upya..
Na siku tukianza kuijadili upya tuhuma hizo, ntamwomba Mh. Rais JPM anipumzishe Uwaziri ili nilishughulikie hili suala kikamilifu.
Tupia Comments: