Leo April 9 2017 Maalim Seif amesema Dola imekuwa ikitumia njama na mbinu chafu ilikuhujumu chama cha CUF kwa kumtumia Lipumba baada ya kumkaribisha Ikulu na kumtumia kushawishi chama hicho kishiriki marudio ya uchaguzi wa march 20 2016….
Akizungumza na waandishi wa habari aliyaongea haya…>>>Njama hizi zilianza mara baada ya kibaraka Ibrahim Lipumba kukaribishwa Ikulu mapema mwaka jana,nyote mnakumbuka sinema ya Lipumba kwanza alitumiwa kutushawishi kushiriki uchaguzi haramu wa marudio wa March 20 2016 huku akiniambia mimi binafsi kuwa nikubali kwani angalau nitaweza kuendelea kuwa makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar’- Maalim Seif
Tupia Comments: