Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeibuka mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Castle Cosafa 2017 baada ya kupata ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Lesotho nchini Afrika Kusini.

Magoli hayo yaliyofungwa kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi kumalizika dakika 90 kwa sare ya bila kufungana.

Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Moruleng, Kipa wa Taifa Stars, Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mashuti mengi yaliyolisakama lango la Stars, ikiwa ni pamoja na kuokoa mkwaju mmoja wa penalti.

Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kupiga mkwaju wa penalti kupitia Shiza Kichuya ambaye alipaisha mkwaju huo.

Hata hivyo, Lesotho nao walipoteza penalti mbili, ambapo moja iligonga mwamba wa pembeni na kutoka nje huku nyingine ikiokolewa na kipa wa Stars, Said Mohamed.

Vijana wa Stars waliofunga mikwaju ya penalti ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda huku Alpha akimalizia mkwaju wa mwisho na kuipa furaha Stars.

Taifa Star imeingia kwenye kusaka nafasi ya tatu baada ya kufungwa na Zambia goli 4-2.

Tupia Comments: