Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameomba radhi baada ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye Ulemavu.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
Mwigulu Nchemba ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge Stella Ikupa lililohoji
Wiki iliyopita mkoani Dar es salaam lilitokea tukio la kusikitisha dhidi ya watu wenye ulemavu ambao ni waendesha bajaji ambapo walifanyiwa vitendo vya udhalilishaji pamoja na vitendo vya kinyama walipigwa sana na baadae kuburuzwa chini. Pamoja na makosa ambao walidaiwa kuwa nayo lakini approach ambayo ilitumika na Askari wetu haikuwa nzuri kabisa, Je nini kauli ya Serikali kwa hili?
“Kwanza naomba ni appologize (niombe radhi) kwa niaba yake,kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba pamoja na utaratibu kuwepo na ukiukwaji wa utaratibu kwa kuzingatia hali yao ni nguvu kubwa imetumika lakini niseme tu sisi kama Serikali tumeshajadiliana na wenzetu wa TAMISEMI watakutana na Wizara ya TAMISEMI pamoja na wenzao wa ngazi ya mkoa ili kuweka utaratibu ambao utakuwa una taswira nzuri na kufanya jambo hilo lisiweze kujirudia kuweka utaratibu wa kudumu,” alisema Mwigulu Nchemba.
Tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam Jeshi la Polisi lilitumia nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuwasilisha malalamiko dhidi ya Askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katika jiji.
Tupia Comments: