Habari iliyopo South Africa ni kwamba wanataka kubadilisha jina la nchi yao, wakidai jina South Africa sio jina bali linaeleza mahali nchi ilipo katika bara la Afrika. Kimsingi wanasema South Africa ni nchi ambayo haina jina.

Wanasema kwamba walipaswa waige mfano wa nchi kama Zimbabwe na Namibia, zilizobadili majina mara baada ya kupata uhuru.

Wazo hili limekuwa likiungwa mkono na vyama mbalimbali vya siasa nchini humo, na maoni ya ANC, chama tawala nchini humo, ni kwamba linapaswa kujadiliwa rasmi katika ngazi za juu za chama.

Kumekuwa na mapendekezo na upendezi kwamba South Africa ibadili jina na kuitwa Azania, jina ambalo huko nyuma lilitumika na vyama kama Pan African Congress (PAC).

Ikiwa South Africa itabadili jina na kuwa Azania, basi itazidi kufanana na Tanzania katika jina, bendera na wimbo wa taifa. Sijui hili limetokeaje.

Source: The Mercury, South Africa

Tupia Comments: