Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imeamuru kuwa kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma inaweza kufanywa kwa siri.
Akitoa uamuzi huo Jaji mkuu Mgoeng Mgoeng alisema kuwa spika wa bunge ana mamlaka ya kuamua ni njia gani kura hiyo itafanyika.
Bwana Zuma amekuwa chini ya shinikizo kufuatia shutuma nyingi ikiwemo madai ya ufisadi na mabadiliko kwa baraza la mawaziri yaliyokumbwa na utata.
Vyama vya upinzani vinaamini kuwa chini ya kura ya siri, wabunge kutoka chama cha Zuma cha ANC wanaweza kupiga kura ya kumpinga.
Spika wa bunge Baleka Mbete alikuwa amedai kuwa sheria za bunge haziruhusu kufanyika kura ya siri lakini sasa itatagazwa tarehe mpya ya kura hiyo.
Tupia Comments: