Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi vigogo wawili hadi uchunguzi wa sakata la vitabu vya kufundishia utakapokamilika.
Waliosimamishwa ni Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu (TIA) ambayo ndiyo imepewa idhini ya kusimamia ubora wa vitabu.
Kauli hiyo imetolewa bungeni jana (Jumatatu) kutokana na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Esther Mmasi kutoa hoja ya kushika shilingi katika mshahara wa waziri akitaka uamuzi kuhusu suala hilo.
Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa kambi zote bungeni wakiwamo, Philipo Mulugo (Songwe -CCM), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini -CCM), Suzan Lyimo (Viti Maalumu -Chadema) na Mwita Waitara (Ukonga -Chadema).
Profesa Ndalichako akijibu hoja hizo, amesema ameunda tume kuchunguza suala hilo na kuwahakikishia kuwa waliohusika hawako katika taasisi ya TIA.
“Nawahakikishia kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi kila aliyehusika atabeba msalaba wake,” amesema.
Tupia Comments: